KARIBUNI KIWANJA

Tuesday, September 28, 2010

AJIUA KWA KUITWA SHOGA

mkazi wa kinondoni ajinyoga kwa kuitwa 'shoga'.!MKAZI wa Kinondoni Deogras Paul (39) amekutwa chumbani kwake akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka kwa kile kilichodaiwa kuitwa hanithi ‘shoga’ na majirani zake.Akizumguza na wandishi wa habari leo , Kamanda wa Polisi Mkoa Kinondoni, Elias Kalinga alisema kuwa, tukio hilo lilitokea jana huko maeneo ya Kinondoni majira ya saa moja kasoro robo ya jioni, alikutwa humo akiwa amejinyonga.Kamanda Kalinga aliendelea kusema kuwa, marehemu alikuwa amejinyonga kwa kutumia shuka hiyo aliyoitundika kwenye dali ya chumba hicho na kupelekea kifo chake, hata hivyo walipopekua walimkuta ameacha ujumbe uliosema kuwa; “Mimi sio shoga, ninafamilia na mtoto, Mungu shahid”, ilieleza sehemu ya maelezo ya ujumbe huo.Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na upelelezi juu ya tukio hilo bado unaendelea.

Wednesday, August 25, 2010

FAIDA ZA KUFUNGA

Umekuwepo mjadala wa kisayansi wa muda mrefu kuhusu kufunga kama kuna manufaa kwa afya ya mtu ama la. Kufunga ni sehemu muhimu ya imani nyingi za kidini, kuanzia Waislamu, Wakristo hadi Wayahudi. Wengi wana mashaka kama faida ya kiroho inayopatika kutokana na funga huwa na uhusiano na afya ya mwili.




Jumuiya nyingi za wataalamu wa tiba mbadala, wanaamini kwamba funga inaweza kufanya maajabu makubwa katika mwili wa binadamu. Katika makala haya, tutajaribu kuangalia hoja zinazotolewa na wataalamu hao wa tiba mbadala katika jitihada za kuihabarisha jamii umuhimu wa funga kiafya.



Kitaalamu, funga huanza kufanya kazi ndani ya saa 10 za kwanza hadi saa 24. Kwa sababu ili athari za funga zianze kuonekana ni mpaka akiba ya wanga iliyomo mwilini inapoanza kutumika kama chanzo cha nishati. Mtu huanza kusikia njaa, pale akiba ya protini inapokwisha mwilini kama nishati.



Kwa kawaida, mwili huwa na uwezo wa kijisafisha wenyewe kwa kutoa sumu mwilini (Detoxification) na hii ndiyo hoja kubwa inayotumiwa na wataalamu wa tiba mbadala wanaoamini funga ni tiba na kinga ya maradhi mengi. Detoxification ni mchakato wa mwili kuua na kutoa sumu mwilini kupitia haja kubwa, ini, figo, mapafu na kwa njia ya ngozi (jasho, n.k).



Faida nyingine ya funga inayoelezewa ni ule mchakato wa uponyaji unaofanyika mwilini wakati mtu anapokuwa amefunga. Inaelezwa kuwa wakati wa funga, ile nishati inayoelekezwa kwenye mfumo wa usagaji chakula, huelekezwa kwenye mfumo wa ‘metabolizi’ na mfumo wa kinga ya mwili. Katika kipindi hicho, magonjwa na mauvimbe ya ajabu ajabu huweza kudhibitiwa na hatimaye kutoweka kabisa.



Vile vile ukarabati wa seli zilizoathirika huko nyuma, huweza kutengenezwa upya na kuwa imara zaidi. Mwisho, faida kubwa iliyothibitishwa kisayansi itokanayo na funga, ni kwamba mtu anayefunga, mwili wake huimarika na miaka yake ya kuishi huongezeka! Faida hii inatokana na ukweli kwamba wakati wa funga uzalishaji wa protini mwilini huwa mkubwa, kasi ya ‘metaboliz’ hushuka, mfumo wa kinga ya mwili huimarika zaidi.



Kuongezeka kwa uzalishaji wa homoni za mwili ndiko kunakochangia faida hizi za muda mrefu. Pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa homoni za ukuwaji wa mwili, homoni za kuzuia uzeekaji wa mwili nazo huzalishwa kwa wingi wakati wa funga, hivyo kumfanya mtu anayefunga mara kwa mara kuonekana kijana kila siku.



Kwa kuhitimisha, inaonekana kuna sababu nyingi za msingi za kuamini kuwa funga ina faida nyingi kwa afya ya binadamu. Hata hivyo, bado kuna baadhi ya madaktari wengine hukataza watu kufunga kwa muda mrefu bila kupata ushauri wao kwa madai kuwa kufunga kuna madhara katika afya, na hii imetokana na ukweli kwamba jamii imekuwa ikiamini kwamba ili mtu uishi unahitaji kula, iweje leo mtu usipokula utaishi sana? Lakini wanasahu kuwa Mungu aliyetuamrisha kufunga anajua zaidi yetu!

Mwana FA & AY ft, Hardmad - Dakika Moja (BONGO STAR LINK - www.djchoka.b...

Sunday, August 1, 2010

MDAU ALETA VURUGU KATIKA KAMPENI YA SHY ROSE BHANJI

Wasimamizi wa mkutano wa wanachama wa CCM Kata ya Kigogo, Dar es Salaam wakimtoa nje ya ukumbi mmoja wa mwanachama aliyesababisha vurugu kutokana na kumuuliza swali la utatanishi mgombea, Shyrose Bhanji (kushoto) wakati wa mkutano wa kuomba kura wa wagombea Ubunge jimbo la Kinondoni, uliofanyika kwenye kata hiyo jana

AJALI YA BASI KAHAMA... ANGALIA UBORA WA MABASI YETU YA ABIRIA ULIVYO


Waokoaji wakitafuta maiti ndani ya Fuso.Picha zote kwa Msaada wa Wanabidii


------

Ajali ya Kanegele - Fuso na Super Najimunisa Kahama Mkoani Shinyanga jana kama unavyoona picha mbalimbali zilizochukuliwa eneo la tukio mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo inayodaiwa kusababisha vifo vya watu 18 . Cha ajabu ajali imetokea mita 10 kutoka katika kizuizi cha askari wa maliasili wanaokagua mazao ya maliasili.Katika ajali hiyo inasemekana askari aliyekuwa akisindikiza basi hilo alikatwa kicha baada ya fuso kuharibiwa vibaya na basi. hebu Jionee mwenyewe picha zilizopigwa katikaajali eneo la tukio huko Kanegele kama inavyoonekana Sura ya Basi la Super Najimunisa baada ya Ajali.

Tuesday, July 27, 2010

MSIBA ROMA MMAKUA KUANGWA JUMAMOSI


Marehemu Hamisi Abdallah George MmakuaKamati kuu ya maandalizi ya kusafirisha mwili wa Marehemu Hamisi Abdallah George(Mmakua) aliyefariki mjini Rome, Italy tarehe 18 julai 2010, saa tatu na dakika ishirini na tano usiku (21:25), ikishirikiana na Jumuiya mbalimbali za Watanzania nchini Italy, inapenda kuwafahamisha Watanzania wote mliopo nchini Italy kuwa mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumamosi tarehe 31 Julai 2010 saa sita mchana(12:00) kabla ya kwenda kupumzika kwa amani nchini Tanzania. Mwili utaagwa kwenye Istituto Lazzaro Spallanzati, iliyopo nyuma ya Ospitali ya San Camillo, kwenye mtaa wa Via Folchi 6/a, mjini Roma. Watanzania wote mnaombwa mfike ili tumuombee na tumuage marehemu. asanteni

JISAMAKI LAVULIWA NUNGWI

Wachukuzi wa samaki katika marikiti kuu ya samaki Darajani wakimshusha samaki aina ya 'Nduaro' aliyevuliwa kijiji cha Nungwi akiwa na uzito wa zaidi ya kilo 150 na ambaye ameuzwa kwa shillingi 1.5m/- katika soko la Nungwi. Chini wakimkatakata vipande samaki huyo baada ya kumpara.

Friday, July 23, 2010

JUMA NATURE KWELI NI MWANA WAFANI ZOTE MPAKA KWENYE USUAI PIA


Nyota wa Bongo Flava Kassim Kiroboto aka Juma Nature(aliyesimama) akijaribu kusuka nyewle msanii mwezanke CPWAA kutoka Park Lane .Ni miaka mitatu iliyopita Leaders Club Kinondoni jijini Darisalaam. Licha ya ususi huu , C-PWAA ni msanii ambaye huwa anapenda kusuka nywele zake kwa mitindo tofauti tofauti.

PATA UJUMBE TOKA KWA KIJANA ROMA

MTOTO MZUNGU AZALIWA KATIKA FAMILIA YA WATU WEUSI


ONDON,Uingereza.WAZAZI wa mtoto aliyezaliwa mzungu nchini Uingereza wamekubali uamuzi wa wataalamu wa vina saba kumfanyia uchunguzi mtoto huyo.Habari kutoka nchini humo zimeeleza kuwa wazazi hao Benjamin na Angela wamekubali mtoto huyo wa kike afanyiwe uchunuzizaidi ili kuibaini sababu za kuzaliwa akiwa katika hali kama hiyo.Mtaalamu wa vina saba kutoka Chuo Kikuu cha London Dkt.Mark Thomas amesema kuwa ana wasiwasi huwenda kuna mchanganyiko wa chembechembe nyeupe na zile na zile zinasobabbisha mtu kuwa na ulemavu wa ngozi albino.Baba mzazi wa binti huyo Benjamni kwa upande wake amesema kuwa lichabya kukubali matokeo ya jinsi mtoto huyo alivyo,bado wataendelea kutafuta sababu za mtoto huyo kuzaliwa hivyo.Mtoto huyo alizaliwa na wazazi weusi ambao ni raia wa Uingereza wenye asili ya Nigeria na inaelezwa kuwa katika familia yao hawana historia ya kuzaliwa mtu wa aina kama hiyo.Benjamin ambaye ni mshauri wa huduma kwa wateja alisema kuwa alipomuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza alishtuka lakini baadaye akasema kuwa ni mwanaye na anamuamini sana mkewe.Alisema mkewe ni mwaminifu kwake sana na walihamia nchini humo wakitokea Nigeria miaka mitano iliyopita. BBC.

Wednesday, July 21, 2010

MSIBA ITALIA

tunatangaza  kifo cha marehemu Hamis George Abdalah ajulikanae na wengi kama Mmakua kilichotokea siku ya jumapili 18/07 jioni pale kwenye hospitali ya San Camillo na kujadili namna ya kuraise fund za kuwezesha usafirishwaji wa mwili wa marehemu kwenda nchini Tanzania kupumzika kwa amani.

HONGERA DADA ZUHURA SAPI KWA KUPATA SHAHADA YA JUU KATIKA CHUO KIKUU CHA LEICESTER NCHINI UINGEREZA

Zuhura Sapi akiwa na Mumewe Kenny Ubah na binti yake Steffy na mtoto wake wa kiume Odi
chini  Zuhura akiwa katitika picha ya pamoja na ndungu na jamaaa

Saturday, July 17, 2010




Ndugu Watanzania,Tumepata habari za kuaminika kutoka vyombo vya habari kutoka Marekani na WHO kwamba wanasayansi nchini Marekani wamegundua chembechembe za kinga ambazo zinauwezo mkubwa wa kupambana na kuua virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ambao hadi sasa hauna chanjo wala tiba ya uhakika.Ugunduzi huo tayari umethibitishwa na wataalamu mbalimbali, ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani.Vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa vimeripoti kuhusu ugunduzi huo ambao unaelekea kutoa mapambazuko mapya kwa ugonjwa huo hatari ambao umekuwa ukiathiri nguvu kazi sehemu mbalimbali duniani, hususan nchi zinazoendelea.Wanasayansi hao wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaida) walieleza katika taarifa yao ya wiki iliyopita kuwa kwenye utafiti huo wamebaini aina mbili za chembechembe zinazoweza kumsaidia binadamu kupambana na virusi vya ukimwi.Mkurugenzi wa Niaida, Dk Anthony Fauci alizitaja chembechembe hizo za kinga kuwa ni VRCO1 na VRCO2 ambazo utafiti wake umeonyesha kuwa zinaweza kuua virusi vya ukimwi kwa asilimia 90.Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) dawa huthibitishwa pale uwezo wake wa kupambana na ugonjwa unapozidi asilimia 60.Dk Fauci alisema hayo ni mafanikio makubwa ya kisayansi tangu wataalamu mbalimbali duniani waanze kufanya utafiti wa namna ya kutibu ugonjwa huo.Alisema chembechembe hizo za kinga hizo VRCO1 na VRCO2 zinaweza kutumika katika kubaini aina mpya ya chanjo ambayo itamuwezesha binadamu kuwa na kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi.Kwa namna chembechembe hizo zinavyofanya kazi, alisema, zikitumika kama chanjo, mwili wa anayechanjwa unajenga kinga ambayo inavishambulia virusi vya Ukimwi na kuviua.“Kwa sasa soko lina dawa za kupunguza nguvu na kasi ya virusi vya Ukimwi kuathiri chembechembe nyeupe za kujikinga na maradhi na hakuna tiba,” alisema Dk Fauci.