Thursday, April 29, 2010
FULHAM - ATLETICO MADRID KUUMANA KATIKA FAINALI KOMBE LA ULAYA
Leo hii Atletico Madrid wamefanikiwa kuingia kaika Fainali ya ligi ya ulaya baada ya kupata goli moja (1) la ugenini zidi ya Liver pool ambayo walishinda magoli 2-1 katika mchezo uliocheza kwa dakika 120 baada ya Liverpool kushinda kwa goli moja, hivyo iliwabidi waende katika muda wa nyongea ndipo Benayoun alipofunga goli la pili, na katika dakika za majeruhi ya kipindi cha pili cha nyongeza ndipo mshambiliaji hatari wa Atletico Madrid aliweza kufunga goli lililo iwezesha Atletico kwenda katika Fainali huko Amburg ujerumani mwezi ujao tarehe 12/5/2010.
USIJE MJINI TUMEJAA EEEH USEMI WA AY NA BINAMUU
Tungo zao mara nyingi zimekuwa na tabia ya kugeuka na kuwa misemo ya mjini,gumzo la mitaani na hata kutumiwa “kibiashara” na makampuni kadhaa ya biashara. Bila shaka unakumbuka chanzo cha misemo kama vile Habari Ndio Hiyo,Nangoja Ageuke, Unaoa lini:Bado nipo nipo,Bed and Breakfast nk
Ni vijana ambao mpaka hivi sasa wanaweza kusema ‘wana mafanikio” fulani kutokana na kazi zao za muziki.Walianzia East Coast na mara kundi hilo lililokuwa na makazi yake pale Upanga-Dar-es-salaam,liliposambaratika wao wameendelea kuwa pamoja kama marafiki na pia wasanii wanaoshirikiana.
Tunawaongelea Mwana FA na A.Y ambaye siku chache zilizopita alipata tuzo ya Teenz kutoka nchini Kenya kama Favourite Artist wa East Africa. Safari hii wimbo unaitwa Usije Mjini. Kwanini nisije mjini wakati mjini nasikia ndio mambo yote? Kila mtu anataka kuja mjini.Mjini hata kwa kuuza maji tu unaweza kujipatia kipato.Mjini kuna starehe zote…inaaminika. Sasa kwanini A.Y na Mwana FA wanasema Usije Mjini? Sikiliza kwa makini tungo hizi
AJALI YA FUSO TANGA YAUA 18 TANGA
Wanafunzi wapatao kumi na nane(18) wamepoteza maisha na wengine mia ishirini na tano (125) kujeruhiwa vibaya sana katika ajali iliyotokea mjini Tanga leo hii, Wanafunzi hao wa chuo cha Shamsil-Maarif Duga Tanga waliokuwa wamepakiwa kwenye Loli aina ya Fuso wakitokea kwenye maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamad S.A.W yaliyofanyika katika kijiji cha Kibafuta
INTER YAINGIA FAINALI ZA UBINGWA WA ULAYA BAADA YA MIAKA 38
Ni furaha kubwa na ya kihistoria kwa timu ya Fc Inter Milan kitika usiku wa jana kwenye uwanja wa Camp nou, baada ya kufanikiwa kuisimamisha mabingwa watetezi Fc Barcelona ambayo ilishinda kwa taabu kwa goli 1-0 lililofungwa na mlinzi wa timu ya Barcelona Pique katika kipindi cha pili cha mchezo huo ambao timu ya Inter ilicheza kwa saa nzima watu kumi uwanjani baada ya mchezaji wao Thiago Motta kutolewa kwa kupewa kadi mbili za njano katika dakika ya 14 ya kipindi cha kwanza, Sasa Inter itakumbana na Bayern Munich kwenye fainali zatakazo fanyika Spain katika mji wa Madrid tarehe 22/5/2010 kwenye uwanja wa Bernabeu.
Wednesday, April 28, 2010
JE INTER WATAISIMAMISHA BARCELONA LEO CAMP NOU?
Jion hii katiaka uwanja wa camp nou kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ta Fc Barcalona na
Fc Inter katika nusu fainali ambayo wengi wa wapenzi wa soka duniani wanadai ni fainali ya kuanzia,
katika pambano hili ambalo wenyeji Barcalona wamewahaidi wapenzi wao kuwa watalipiza kisasi cha
kufungwa magoli 3-I na Inter katika mechi yao ya awali iliyofanyika wiki moja iliyopita mjini milan.
Tuesday, April 27, 2010
BAYERN WATANGULIA BERNABEU
Mshambuliaji IVICA OLIC ameiwezesha timu yake ya BAYERN MUNICH kuingia fainali za ubingwa wa ulaya baada ya kuifunga timu ya LYON kwa magoli 3-0, magoli yote hayo yalifungwa na mchezaji huyo. Bayern wanasubiri mshindi kati ya BARCA na INTER
WANA JUMUIYA
Viongozi na wanajumuiya wakipata picha ya ukumbusho baada ya kikao cha jumuiya hiyo katika makao makuu ya jumuiya hiyo
MUWAKILISHI MPYA WA JUMUIYA YA WATANZANIA PADOVA
Pichani ndugu ZACHARIA M.MHESSA, siku ya jumamosi 24/04/2010 kwenye mkutano mkuu wa jumuiya ya Watanzania Italia aliteuliwa kuwa katibu mwakilishi wa jumuiya ya Watanzania Italia tawi la PADOVA na VENEZIA.Mwenyekiti aliwataka wawakilishi hao kuitisha mkutano haraka katika majimbo yao kwa ajili ya kuorodhesha watanzania wanaoishi katika maeneo hayo na kusikiliza maoni yao juu ya uboreshaji wa maendeleo ya matawi yao na kujua matatizo ya Watanzania wa sehemu hizo.Mwenyekiti pia aliwataka kuwakilisha taarifa za mikutano na matatizo ya watanzania wa sehemu zao kwa katibu mkuu ndugu Kagutta N.Maulidi.
MUWAKILISHI MPYA WA JUMUIYA YA WATANZANIA GENOVA
Ndugu RICKY JOHNSON GEORGE BONDO pichani ameteuliwa kuwa katibu muwakilishi wa Jumuiya ya watanzania tawi la GENOVA, Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania Italia Mh Abdurahaman A Ali alifanya uteuzi huo katika mkutano mkuu wa Jumuiya uliofanyika tarehe 24/04/2010 jumamosi katika makao makuu ya jumuiya hiyo mjini Napoli
MKUTANO MKUU YA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA
Viongozi na wajumbe wa jumuiya ya Watanzania Italia katika picha ya pamoja baada ya kikao cha mkutano mkuu kilichofanyika mjini Napoli Makao makuu ya jumuiya ya Watanzania Italia. Mkutano huo ulioanza saa nne asubuhi na kusimamishwa kwa mapumziko saa saba mchana, mkutano uliendelea tena na kumalizika saa kumi na moja jioni. Mkutano ulifunguliwa na katibu mkuu wa jumuiya ndugu KAGUTTA N.MAULIDI kwa hotuba yenye mukhtasari mzima wa jumuiya,malengo ya jumuiya,mafanikio na matatizo kwa jumla yanayokabili Watanzania kwa jumla wanaoishi Italia.Mwisho katibu mkuu alitoa shukrani nyingi kwa balozi wa Tanzania ROME Mh. ALI KARUME kwa ushirikiano mkubwa anaoutoa kama mlezi wa jumuiya na Watanzania Italia na kwa Watanzania wote wanaoishi Italia. Jumuiya ya Watanzania imefungua matawi mengine rasmi na kufatiwa na uteuzi wa makatibu wa jumuiya wa sehemu hizo. Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia Mh. Abdulrahaman A.Alli alimteua ndugu RICKY JOHNSON GEORGE BONDO kuwa katibu muwakilishi wa jumuiya ya Watanzania tawi la GENOVA, pia ndugu ZACHARIA MHESA aliteuliwa kuwa katibu mwakilishi wa PADOVA na VENEZIA
Monday, April 26, 2010
MUUNGANO LEO NI MIAKA 46
Rais Jakaya Kikwete(kushoto) akiwapungia mkono wananchi.Kulia ni General Davis Mwamunyange,Mkuu wa Majeshi Tanzania
Saturday, April 24, 2010
Friday, April 23, 2010
FERNANDO TORRES " EL NINO " KUITOKA LIVERPOOL?
Mmiliki wa timu ya Manchester City Sheikh Mansour Bin Zayed yupo tayari kutumia milioni 70 euro, kwa kumnunua mshambuliaji hatari Fernando Torre miaka 26 kutoka Liverpool katika msimu ujao, Pia timu ya Juventus nayo iko mbioni katika mazungumzo na meneja wa mchezaji huyo ambae inasemekana amekuwa hana maelewano mazuri na timu yake hiyo.
Thursday, April 22, 2010
SHEREHE ZA MUUNGANO KUFANYIKA ROME TAREHE 24 APRIL WOTE MNAKARIBISHWA
Sherehe ya Muungano wa Tanzania iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Roma(TZ-RM), itafanyika mjini Roma tarehe 24 April 2010 kwenye ukumbi wa L'Aggiustafesta uliopo Maeneo ya Cassia- Grottarosa kwenye mtaa wa Via Cassalatico 6. Watanzania wote muishio Italia mnakaribisha kujumuika na kusherekea siku hii muhimu kwa Taifa letu. Ukumbi utafunguliwa kuanzia saa nane na nusu na sherehe kuanza Rasmi saa tisa kamili. Tunaomba tujitaidi kufika mapema ili sherehe iende kama ilivyopangwa.kwa maelezo zaidi mnaweza kutuandikia e-mail watanzaniaroma@yahoo.it au kutupigia simu 3479094800. Wote mnakaribishwa.
FULHAM YAIBANA AMBURG
Fulham leo imeweza kujipa matumaini ya kuingia fainali baada ya kuibana timu ngumu Amburg kwa kutoka nayo sare ya bila ya kufungana katika mchezo uliokuwa mkali, Pichani ni beki mahiri wa timu ya Fulham Hughes akiokoa mpira huku Van Nistelrooy akimuangalia
BENITEZ KUTEMA LIVERPOOL?
Kuna uvumi umeenea katika timu kamambe ya Juventus ya mjini Torino kuwa inafanya majadiliano ya chini chini na Kocha wa timu ya Liverpool ili katika msimu ujao aje kuifundisha timu hiyo kwa dau nono la 5mil euro kwa mwaka, mshikemshike ilijaribu kudadisi kwa karibu kupitia kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa timu hiyo ya Juventus ambaye jina lake tumeliifadhi kwa kusema yeye hana tarifa zozote kuhusiana na habari hizo.
L' ATLETICO MADRID VC FC LIVERPOOL
L' Atiletico Madrid usikuu imeifunga Fc Liverpool goli moja kwa bila katika uwanja wa Vicente Calderon, bao hilo la pekee katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji hatari wa timu hiyo Diego Forlan katika dakika ya 9 katika kipindi cha kwanza.
Wednesday, April 21, 2010
BONDE LETU LINA WAREMBO JAMANII
Cheki mwenyewe mrembo kama huyu, kwa mtazamo wangu gharama zake ni hizo baangirii na poda si muhimu sana kwake
J MARTIN MSANII TOKA NIGERIA AKIKAMUA JIJINI DAR
Msanii J.Martin akiwapagawisha wapenzi wa muziki wa Dar na vitongoji vyake usiku huu kwenye makao makuu ya Zain ambao ndio waliomualika Nchini
Tuesday, April 20, 2010
ASHA BARAKA PRODYUZA WA FILAMU YA LOVELY GAMBLE
Yule prodyuza wa Filamu mpya ya Lovely Gamble Dada Asha Baraka akionyesha DVD za filamu hiyo jna
mjini Dar na kwamba uzinduzi maalumu utafanyika April 28-2010 kwenye ukumbi wa Club Billicanas jijini Dar.
Subscribe to:
Posts (Atom)























