Wednesday, July 28, 2010
Tuesday, July 27, 2010
MSIBA ROMA MMAKUA KUANGWA JUMAMOSI
Marehemu Hamisi Abdallah George MmakuaKamati kuu ya maandalizi ya kusafirisha mwili wa Marehemu Hamisi Abdallah George(Mmakua) aliyefariki mjini Rome, Italy tarehe 18 julai 2010, saa tatu na dakika ishirini na tano usiku (21:25), ikishirikiana na Jumuiya mbalimbali za Watanzania nchini Italy, inapenda kuwafahamisha Watanzania wote mliopo nchini Italy kuwa mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumamosi tarehe 31 Julai 2010 saa sita mchana(12:00) kabla ya kwenda kupumzika kwa amani nchini Tanzania. Mwili utaagwa kwenye Istituto Lazzaro Spallanzati, iliyopo nyuma ya Ospitali ya San Camillo, kwenye mtaa wa Via Folchi 6/a, mjini Roma. Watanzania wote mnaombwa mfike ili tumuombee na tumuage marehemu. asanteni
JISAMAKI LAVULIWA NUNGWI
Wachukuzi wa samaki katika marikiti kuu ya samaki Darajani wakimshusha samaki aina ya 'Nduaro' aliyevuliwa kijiji cha Nungwi akiwa na uzito wa zaidi ya kilo 150 na ambaye ameuzwa kwa shillingi 1.5m/- katika soko la Nungwi. Chini wakimkatakata vipande samaki huyo baada ya kumpara.
Friday, July 23, 2010
JUMA NATURE KWELI NI MWANA WAFANI ZOTE MPAKA KWENYE USUAI PIA
Nyota wa Bongo Flava Kassim Kiroboto aka Juma Nature(aliyesimama) akijaribu kusuka nyewle msanii mwezanke CPWAA kutoka Park Lane .Ni miaka mitatu iliyopita Leaders Club Kinondoni jijini Darisalaam. Licha ya ususi huu , C-PWAA ni msanii ambaye huwa anapenda kusuka nywele zake kwa mitindo tofauti tofauti.
MTOTO MZUNGU AZALIWA KATIKA FAMILIA YA WATU WEUSI
ONDON,Uingereza.WAZAZI wa mtoto aliyezaliwa mzungu nchini Uingereza wamekubali uamuzi wa wataalamu wa vina saba kumfanyia uchunguzi mtoto huyo.Habari kutoka nchini humo zimeeleza kuwa wazazi hao Benjamin na Angela wamekubali mtoto huyo wa kike afanyiwe uchunuzizaidi ili kuibaini sababu za kuzaliwa akiwa katika hali kama hiyo.Mtaalamu wa vina saba kutoka Chuo Kikuu cha London Dkt.Mark Thomas amesema kuwa ana wasiwasi huwenda kuna mchanganyiko wa chembechembe nyeupe na zile na zile zinasobabbisha mtu kuwa na ulemavu wa ngozi albino.Baba mzazi wa binti huyo Benjamni kwa upande wake amesema kuwa lichabya kukubali matokeo ya jinsi mtoto huyo alivyo,bado wataendelea kutafuta sababu za mtoto huyo kuzaliwa hivyo.Mtoto huyo alizaliwa na wazazi weusi ambao ni raia wa Uingereza wenye asili ya Nigeria na inaelezwa kuwa katika familia yao hawana historia ya kuzaliwa mtu wa aina kama hiyo.Benjamin ambaye ni mshauri wa huduma kwa wateja alisema kuwa alipomuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza alishtuka lakini baadaye akasema kuwa ni mwanaye na anamuamini sana mkewe.Alisema mkewe ni mwaminifu kwake sana na walihamia nchini humo wakitokea Nigeria miaka mitano iliyopita. BBC.
Wednesday, July 21, 2010
MSIBA ITALIA
tunatangaza kifo cha marehemu Hamis George Abdalah ajulikanae na wengi kama Mmakua kilichotokea siku ya jumapili 18/07 jioni pale kwenye hospitali ya San Camillo na kujadili namna ya kuraise fund za kuwezesha usafirishwaji wa mwili wa marehemu kwenda nchini Tanzania kupumzika kwa amani.
HONGERA DADA ZUHURA SAPI KWA KUPATA SHAHADA YA JUU KATIKA CHUO KIKUU CHA LEICESTER NCHINI UINGEREZA
Zuhura Sapi akiwa na Mumewe Kenny Ubah na binti yake Steffy na mtoto wake wa kiume Odi
Sunday, July 18, 2010
Saturday, July 17, 2010
Ndugu Watanzania,Tumepata habari za kuaminika kutoka vyombo vya habari kutoka Marekani na WHO kwamba wanasayansi nchini Marekani wamegundua chembechembe za kinga ambazo zinauwezo mkubwa wa kupambana na kuua virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ambao hadi sasa hauna chanjo wala tiba ya uhakika.Ugunduzi huo tayari umethibitishwa na wataalamu mbalimbali, ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani.Vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa vimeripoti kuhusu ugunduzi huo ambao unaelekea kutoa mapambazuko mapya kwa ugonjwa huo hatari ambao umekuwa ukiathiri nguvu kazi sehemu mbalimbali duniani, hususan nchi zinazoendelea.Wanasayansi hao wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaida) walieleza katika taarifa yao ya wiki iliyopita kuwa kwenye utafiti huo wamebaini aina mbili za chembechembe zinazoweza kumsaidia binadamu kupambana na virusi vya ukimwi.Mkurugenzi wa Niaida, Dk Anthony Fauci alizitaja chembechembe hizo za kinga kuwa ni VRCO1 na VRCO2 ambazo utafiti wake umeonyesha kuwa zinaweza kuua virusi vya ukimwi kwa asilimia 90.Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) dawa huthibitishwa pale uwezo wake wa kupambana na ugonjwa unapozidi asilimia 60.Dk Fauci alisema hayo ni mafanikio makubwa ya kisayansi tangu wataalamu mbalimbali duniani waanze kufanya utafiti wa namna ya kutibu ugonjwa huo.Alisema chembechembe hizo za kinga hizo VRCO1 na VRCO2 zinaweza kutumika katika kubaini aina mpya ya chanjo ambayo itamuwezesha binadamu kuwa na kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi.Kwa namna chembechembe hizo zinavyofanya kazi, alisema, zikitumika kama chanjo, mwili wa anayechanjwa unajenga kinga ambayo inavishambulia virusi vya Ukimwi na kuviua.“Kwa sasa soko lina dawa za kupunguza nguvu na kasi ya virusi vya Ukimwi kuathiri chembechembe nyeupe za kujikinga na maradhi na hakuna tiba,” alisema Dk Fauci.
Thursday, July 15, 2010
POLISI UGANDA WAKAMATA MKANDA WA MABOMU
Polisi nchini Uganda akionesha mkanda wenye mabomu uliyotumiwa na watu wanaliojitoa mhanga ambao ulikutwa kwenye mfuko wa kubebea kompyuta ndogo aina ya Laptop katika klabu eneo la Makindye. Polisi wanaamini kuwa mkanda huo ambao haukulipuka utawasaisadia kuwabaini wahusika wa milipuko miwili iliyoua zaidi ya watu 70 nchini humo usiku wa Jumapili iliyopita. ( AFP)
ASKARI WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA DAR WANAOGOPA WAZUNGU
MICHUZI
Ankal leo nimepita uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar na kuona maajabu ya dunia. nimeona mapolisi wamevaa kiraia wakisimamisha kila mmatumb anayepita, ila mzungu hata mmoja hajaguswa. ina maana hicho wanachokitafuta kwa wamatumbi wenzao kama unga ama hata zana za ugaidi wazungu hawabebi. mpe salamu saidi mwema na kamanda kova. hii ni hatari sna kuwaachia wazungu na kuwaandama wamatumbi, tena wakiwa wamenuna utadhani hawataki tusafiri
Ankal leo nimepita uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar na kuona maajabu ya dunia. nimeona mapolisi wamevaa kiraia wakisimamisha kila mmatumb anayepita, ila mzungu hata mmoja hajaguswa. ina maana hicho wanachokitafuta kwa wamatumbi wenzao kama unga ama hata zana za ugaidi wazungu hawabebi. mpe salamu saidi mwema na kamanda kova. hii ni hatari sna kuwaachia wazungu na kuwaandama wamatumbi, tena wakiwa wamenuna utadhani hawataki tusafiri
Monday, July 12, 2010
Sunday, July 11, 2010
MSURURU WA MAGARI JIJINI DAR
Kwa muda mrefu sasa jiji la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na tatizo la msongamano wa magari unaowasababishia wananchi kero na hasara za kiuchumi. Hali kama hii imekuwa ni jambo la kawaida na haijafahamika ni lini tatizo hili litakwisha.
Friday, July 9, 2010
Thursday, July 8, 2010
RAISI WA BRAZIL YUKO TANZANIA
MICHUZI
Rais Luiz Lula Da Silva wa Brazil akimuangalia Simba dume aliyekaushwa kwa utaalamu na kuwekwa kama pambo katika mlango wa ikulu jijini Dar
Rais Luiz Lula Da Silva wa Brazil akimuangalia Simba dume aliyekaushwa kwa utaalamu na kuwekwa kama pambo katika mlango wa ikulu jijini Dar
SHYROSE KUGOMBEA UBUNGE KINONDONI
• Asema mwaka 2010 ubunge unahitaji tafsiri mpya• Aainisha maeneo nane atayoyafanyia kazi• Kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana• abainisha umuhimu wa ofisi kila kata ndani ya jimboKada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Sadruddin Bhanji ametangaza kujitosa katika nafasi ya ubunge jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia CCM na lengo lake kubwa ni kuwa kiungo muhimu katika jamii ya wanakinondoni.Akitangaza azma yake ya kuomba ridhaa kwa wanachama wa CCM katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Shy-Rose alisema kwa mtazamo wake neno ubunge kwa mwaka 2010 linahitaji tafsiri mpya kabisa. `…kwa sasa mbunge anatakiwa kuwa ni kiungo cha jamii badala ya kuwa mwakilishi wa jimbo kama ilivyozoeleka` alifafanua Shy-Rose.`Mwaka 2010 ni mwaka wa mabadiliko na ndio maana nimeona kwamba ili kila mwananchi kuweza kuwajibika, nafasi ya mbunge inahitaji kutafsiriwa upya ili iendane na wakati na matatizo ambayo yanayotukakabili wananch` alisema.Kwa maana hiyo amesema kwamba hata sifa za mbunge zinahitaji kutafsiriwa upya kabisa, kwani majukumu yake yamebadilika kuendana na wakati. Ametaja baadhi ya sifa hizo mpya ni kuwa mhamasishaji, kiungo muhimu, kufanya kazi usiku na mchana na kuwa na ofisi katika kila kata ndani ya jimbo husika ili kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi.`naomba nitoe tafsiri mpya ya neno ubunge..mbunge anatakiwa sasa awe ni kiungo muhimu kati ya walio na kipato kikubwa, kipato cha kati na wasio na kipato kabisa ili kwa pamoja jimbo liweze kupiga hatua za kimaendeleo. Mimi nitahakikisha kwamba nina ofisi katika kila kata ili niweze kuwafikia wananchi wangu katika kata zote kwani wakati napita kuomba kura ninawafuata na baada ya kufanikiwa kutimiza azma yangu ni wakati wa kuendelea kuwafuata na si wao kunifuata` alisema.(MICHUZI BLOG)
Wednesday, July 7, 2010
Tuesday, July 6, 2010
Subscribe to:
Posts (Atom)

















































