Monday, May 31, 2010
HAKUNA BIFFU KATI YA BERRY WHITE NA BERRY BLACK
"Juzi nashukuru Mungu nimeweza maliza tofauti kati ya berry white na berry black kwa kuwakutanisha tena katika uzinduzi wa album ya berry black (nafsi yako) na album ya chege (karibu kiumeni) bif ilidumu tokea mwaka 2006 walipotoa wimbo wa mwisho ulioitwa na wewe tu ft.shirkoKwa sasa wapo peace lakini watabaki kila mmoja akifanya kazi kivyake na wanaweza shirikiana,so 2 berry haipo tena watabaki kutumia majina yao b white au b blackWalikuwa hawasalimiani kabisa na walikuwa kama chui na paka kwa sasa kama mnavyoona katika pics wapo peace kabisaNawashukuru sana na Amani idumu baina yao InshallahKuendeleza Zenji Fleva" Guru Ramadhani (kati pichani) ambaye pia ni Meneja wa studio ya Guru Recordz
CROATIA MTOTO WA MIAKA 13 AJIFUNGUA MAPACHA
Mtoto wa miaka 13 nchini Croatia amejifungua mapacha na kijana wa miaka 16, baba wa binti huyo amemfungulia mashitaka kijana huyo kwa kitendo hicho cha kuzaa na binti yake akiwa bado ni mdogo
MOURINHO : SITO HISAHAU INTER
Leo hii Jose Mourinho atangazwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid kwa kipindi cha miaka minne ijayo, katika mkutano wa waandishi wa habari Bernabeu, Mourinho baada ya mafanikio ya kiistoria ambayo aliwezesha timu ya inter ya italia kushinda vikombe vtatu muhimu na kuwa kocha pekee wa kigeni kuishinda katika italia. katika mkutano huo alihaidi kuijenga klabu yake hiyo mpya ili iweze kushinda vikombe vyote muhimu. Kuhusu usajili alisema ya kuwa ni mapema mno kuliongelea swala hilo na kuhaidi kuwa wachezaji waliopo Real Madrid ni wachezaji wa kimataifa na wanauwezo mkubwa wa kufanya vizuri wakiwa chini ya uongozi wake.
Sunday, May 30, 2010
UMOJA NI NGUVU
Kama tunaweza kushikamana na kuungana kwa pamoja kama watoto hawa watanganyika tunaweza kufika mbali sana. Umoja ni Nguvu Daima!!!
KIKONGWE
Pamoja na umaskini mkubwa unaolikabili Bara la Afrika na Waafrika kwa ujumla wapo wanaobahatika kuishi muda mrefu zaidi.
ACTOR DENNIS HOPPER 74 AFARIKI
Actor Dennis Hopper amefarika dunia nyumbani kwake Venice California siku ya jumamosi 29 may 2010 alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa muda mrefu, pichani dennis hopper akiwa na jack nicholson wakati wa uhai wake
MASHOGA MALAWI WAPATA MSAMAHA WA RAISI
Wale mashoga wawili waliofungwa miaka 14 Stephen Monjenza miaka 26 na Tiwonge Chiwalamba miaka 20 wamepata msamaha kutoka kwa Rais Bingu wa Mutharika, mashoga hao walikamatwa na kutiwa hatiani baada ya kusheherekea ndoa yao kiendo ambacho kulichukuliwa na serikari kuwa ni cha kuvunja sheria, Msamaha huo wa Rais Bingu aliutoa baada ya ziara ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa ndugu Ban ki Moon, mashoga hao waliachiwa jumamosi jioni baada ya msamaha kutolewa, hata hivyo waziri moja wa serikali aliifahamisha mshikemshike kuwa iwapo wataendelea na vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali kisheria zitatumika
Saturday, May 29, 2010
MLIPUKO KATIKA HANDAKI WAUA WATU 6 GAZZA NA EGYPT
Mlipuko umetokea jumamosi hii katika mahandaki ya chini kwa chini kati Gazza na Egypt na kuua watu sita na 12 kujeruhiwa, mpaka sasa uchunguzi unaendelea ili kujua chanzo cha mlipuko huo.
MOURINHO KOCHA MPYA WA REAL MADRID
Klabu ya Real Madrid ya Uhispania imetangaza kwamba itamjulisha Jose Mourinho rasmi kwa mashabiki wao, Jumatatu ijayo.
Mourinho atajulishwa kwa mashabiki wa Real siku ya Jumatatu
Klabu kilitoa taarifa kuthibitisha hayo.
Marais wa vilabu vya Inter Milan ya Italia, na Real Madrid, walikutana Ijumaa mjini Milan, Italia, kutatua masuala yote, hasa ya kifedha, kuhusiana na Jose Mourinho kuhama kutoka Inter, na kuelekea Uhispania.
Real Madrid wameshawahi kunyakua ubingwa wa Ulaya mara tisa.
Jose Mourinho anaondoka Inter baada ya msimu uliokuwa wa fanaka mno, kupata ushindi katika mashindano matatu muhimu Italia, ikiwa ni pamoja na kuwa klabu bingwa barani Ulaya.
Hata hivyo klabu ya Inter haikutoa maelezo kamili katika taarifa hiyo, kuhusu mapatano hayo kati ya rais wa klabu Massimo Moratti na mwenzake wa Real, Florentino Perez.
Lakini vyombo vya habari nchini Uhispania vimekuwa vikielezea kwamba Inter watapata euro milioni nane, ambazo ni sawa na dola milioni 9.80.
Mourinho aliiongoza Inter kupata vikombe vitatu muhimu, na alimalizia kwa ushindi katika fainali ya klabu bingwa Ulaya, dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani katika uwanja wa Bernabeu, mjini Madrid
YALIYOJIRI JANA PALE MZALENDO PUB NA MACHOZI BAND.
Jana ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa Machozi Band kutumbuiza pale Mzalendo Pub baada yakutoka ZHONG HUA GARDEN walipokuwa wanapiga kila ijumaa. Kuanzia jana ijumaa na ijumaa nyingine utakuwa unawapata Machozi Band pale Mzalendo Pub
MPIGANAJI
Mie nadhani huyu kuku kama angekua anaongea basi anamengi ya kusimulia mana amepigana vita nyingi kianzia kwa kuku wenzaka mpaka kukoswa koswa kuchinja na bado anadunda
MCHEZO WA UTELEZI
Wanafunzi wa shule ya Msingi wakicheza mchezo wa kuteleza katika eneo la ngazi za kupandia kwa miguu zilizopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam huku mvua ikinyesha jana.Picha na Fadhili Akida
Friday, May 28, 2010
MZEE PWAGU AFARIKI DUNIA
Mzee Rajabu Hatia almaharufu kama Mzee Pwagu, amefariki dunia jioni hii katika hospitali ya mwananyamala jijini Dar katika majira ya saa kumi za jioni alikokuwa amelazwa kwa maradhi yaliyokuwa yamemsumbua kwa muda mrefu. mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho katika makaburi ya kigogo jijini Dar.
msiba upo nyumbani kwake kigogo karibu na round about ya kigogo na magomeni.
50 CENT NA MOVIE MPYA
Lile Rapa mashuhuri na mcheza sinema Curtis Jackson anafahamika kama 50 cent akiwa katika mtazamo mpya kabisa ambao ataonekana katika filamu anayojiandaa nayo kama mgonjwa wa saratani.
MTIHANI WA DARASA LA PILI
MTIHANI WA MAARIFA YA DUNIA:
instruction, muda 10 seconds
majibu mpe mwenzako
JIBU MASWALI YOTE
1. Kama hela haioti kwenye miti kwa nini banki zina matawi?
2. kwa nini gundi hazigandi kwenye chupa yake?
3. Kama tunatakiwa tusi-drive wakati tumekunywa,kwanini bar kuna parking?
4 . Kama tunatakiwa kufanya sex ndani ya ndoa tu,kwanini tunabalehe kabla ya kufunga ndoa?
Best wishes.
instruction, muda 10 seconds
majibu mpe mwenzako
JIBU MASWALI YOTE
1. Kama hela haioti kwenye miti kwa nini banki zina matawi?
2. kwa nini gundi hazigandi kwenye chupa yake?
3. Kama tunatakiwa tusi-drive wakati tumekunywa,kwanini bar kuna parking?
4 . Kama tunatakiwa kufanya sex ndani ya ndoa tu,kwanini tunabalehe kabla ya kufunga ndoa?
Best wishes.
Thursday, May 27, 2010
Wednesday, May 26, 2010
MTRAKATIFU NYERERE
Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,hivi karibuni atajulikana kama Mtakatifu Julius Kambarage Nyerere au kwa kiingereza Saint Julius K.Nyerere
JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI YA KAKAMAA
Rais Mwai Kibaki wa Kenya akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Kikwete katika ikulu ya Nairobi ambapo viongozi hao wawili walifanya mazungumzo mafupi kabla ya Rais Kikwete kulihutubia bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Picha na Freddy Maro/Ikulu
WATALII WAKIWA NJIANI SOUTH
"Kiongozi wa msafara wa mashabiki wa soka wanaolekea afrika ya kusini kushuhudia kombe la dunia Bw. John Inden [katikati]akiwa ndani ya kreta ya mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro[ncaa] mara baada ya kucheza soka la kuhamasisha na wenyeji wa eneo kutoka kushoto ni kijana wa jamii wa wafugaji wa kimasai leboi meeshaa,meneja wa uhusiano wa ncaa adam akyoo na mkurugenzi wa masoko wa bodi ya utalii nchini."
Tuesday, May 25, 2010
FERRI DAR
Wavuvi wa samaki katika Soko la Magogoni, Dar es Salaam wakiuza kitoweo hicho kwa wachuuzi baada ya kurejea kutoka kuvua. Kwa sasa samaki wadogo ndio wanaopatikana kwa wingi sokoni hapo.
MAAFA YA MOTO KIGAMBONI
Baadhi ya wakazi wa Vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam wakiangalia mabaki ya chumba walichofia watu watano wa familia moja baada ya chumba hicho kuchomwa moto usiku wa manane wakati wakiwa wamelala na kuteketea juzi. Wadau wa kigamboni poleni
BRAZIL KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI NA TANZANIA NA ZIMBABWE
Maandalizi makubwa yameanza kutayarishwa kwa ujio wa timu ya taifa ya Brazil itakayokipiga na timu ya Taifa stars siku ya tarehe 2/6/2010 katika uwanja mpya wa national jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea south tayari kwa game lao la ufunguzi na timu ya Portugal huko Durban juni 25, 2010.Pia chama cha mpira cha Brazil kimesema kuwa juni 7, 2010 timu hiyo itakuwa mjini Harare kwa kukipiga na timu ya Zimbabwe kabla ya kuelekea nchini South Africa.
Monday, May 24, 2010
ADRIANO KUJIUNGA NA ROMA
Adriano mchezaji wa zamani wa mabingwa wa ulaya Fc Inter na Flamengo ya Rio de Jenairo anampango wa kujiunga na AS Roma kwa msimu ujao wa ligi ya seria A, makubaliano ya roma na flamingo yapo katika hatua za mwisho inawezekana baada ya siku tatu zijazo Roma wanaweza kutiliana mkataba na mjezaji huyo
VAZI LA SERENA ?
Ilikuwa ndiyo ufunguzi wa mashindano ya French ambapo Mcheza tenis maarufu Serena alivofanya watu waangalie kivazi alichovaa instead of mchezo wake zidi ya mpinzani Patty…Kama uonavyo katika picha..
mlinda mlango wa zamani wa Arsenal David Seamen Mlima Kilimanjaro
David Seamen akiwa na waongoza watalii wa kampuni ya Zara Adventure mlima Kilimanjaro walikopanda Mei 19 kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kituo cha watoto cha Donna luis Hospice ch a nchi Uingereza
DOGO DIAMOND ACHEZEA MAKOFI IRINGA
J
Mshindi wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010 Diamond alipokea kichapo nje ya ukumbi wa st.dominic Iringa baada ya kutaka kumpiga DJ Muba na msanii wa vichekesho Athuman Mussa a.k.a Mwalubadu .Diamond alifikia hatua hiyo ya kufanya fujo kubwa katika ukumbi huo baada ya kumaliza kuimba na kushuka jukwaani na akiwa nje ya ukumbi huo alimtukana matusi ya nguoni kwa kutumia ishara ya kidole Mbarouk Salum maarufu kama DJ Muba ambaye alikuwa akipinga muziki katika ukumbi huoHatua ya msanii huyo kumtukana DJ Muba ilionyesha kuwakwaza mashabiki wa DJ huyo ambao wamekuwa wakimtegemea katika tasnia ya burudani ndani ya mkoa wa Iringa kwa kupitia kituo cha Radio Ebony Fm na ukumbi wa club V.I.P wa mjini hapo, hali iliyopelekea mashabiki hao kuanza kumshambulia msanii huyo Diamond kwa kumwita mchanga sana katika sanaa hiyo na kuwa tuzo ya Kilimanjaro isimfanye matawi ya juu pamoja na kumweleza ukweli kuwa DJ Muba ni maarufu mara 100 kwake hivyo asitake kujifanyanisha na DJ huyo kauli zilizomkwaza msanii huyo Diamond.
Mshindi wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010 Diamond alipokea kichapo nje ya ukumbi wa st.dominic Iringa baada ya kutaka kumpiga DJ Muba na msanii wa vichekesho Athuman Mussa a.k.a Mwalubadu .Diamond alifikia hatua hiyo ya kufanya fujo kubwa katika ukumbi huo baada ya kumaliza kuimba na kushuka jukwaani na akiwa nje ya ukumbi huo alimtukana matusi ya nguoni kwa kutumia ishara ya kidole Mbarouk Salum maarufu kama DJ Muba ambaye alikuwa akipinga muziki katika ukumbi huoHatua ya msanii huyo kumtukana DJ Muba ilionyesha kuwakwaza mashabiki wa DJ huyo ambao wamekuwa wakimtegemea katika tasnia ya burudani ndani ya mkoa wa Iringa kwa kupitia kituo cha Radio Ebony Fm na ukumbi wa club V.I.P wa mjini hapo, hali iliyopelekea mashabiki hao kuanza kumshambulia msanii huyo Diamond kwa kumwita mchanga sana katika sanaa hiyo na kuwa tuzo ya Kilimanjaro isimfanye matawi ya juu pamoja na kumweleza ukweli kuwa DJ Muba ni maarufu mara 100 kwake hivyo asitake kujifanyanisha na DJ huyo kauli zilizomkwaza msanii huyo Diamond.
Dr KINYAU NYAU AKIFANYA VITU VYAKE
Nikiwa kama DR. Manyaunyau bingwa wa tiba hasili Africa Mashariki, Kwa wale wenye matatizo ya kisukari, Pumu, kusafisha nyota, Kupata strok, Nguvu za kiume na Kutoa vitu kwenye majumba na mitaani pia.
Wasiliana nami kupita namba 255 755 631291 begin_of_the_skype_highlighting 255 755 631291 end_of_the_skype_highlighting,
Email: manyaunyau@yahoo.com
www.drmanyaunyau.blogspot.com
Sunday, May 23, 2010
Saturday, May 22, 2010
MISS USA ANA ASILI YA KIARABU
Miss USA mwenye asili ya kilebanon Rima Fakih mwenye miaka 24, kama kawaida ya jumuiya za kiarabu wameshakemea kwa binti huyo kuwa miss USA
MILITO NIGHT
Price Diego milito ameweza kuipatia timu yake ya Inter Milan magoli mawili na kuiwezesha kulitwaa kombe la ubingwa wa ulaya kwa vilabu dhidi ya timu ta Bayern Munich jumamosi hii baada ya miaka 45 iliyopita
Subscribe to:
Posts (Atom)














































