KARIBUNI KIWANJA

Tuesday, April 27, 2010

MKUTANO MKUU YA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA

Viongozi na wajumbe wa jumuiya ya Watanzania Italia katika picha ya pamoja baada ya kikao cha mkutano mkuu kilichofanyika mjini Napoli Makao makuu ya jumuiya ya Watanzania Italia. Mkutano huo ulioanza saa nne asubuhi na kusimamishwa kwa mapumziko saa saba mchana, mkutano uliendelea tena na kumalizika saa kumi na moja jioni. Mkutano ulifunguliwa na katibu mkuu wa jumuiya ndugu KAGUTTA N.MAULIDI kwa hotuba yenye mukhtasari mzima wa jumuiya,malengo ya jumuiya,mafanikio na matatizo kwa jumla yanayokabili Watanzania kwa jumla wanaoishi Italia.Mwisho katibu mkuu alitoa shukrani nyingi kwa balozi wa Tanzania ROME Mh. ALI KARUME kwa ushirikiano mkubwa anaoutoa kama mlezi wa jumuiya na Watanzania Italia na kwa Watanzania wote wanaoishi Italia. Jumuiya ya Watanzania imefungua matawi mengine rasmi na kufatiwa na uteuzi wa makatibu wa jumuiya wa sehemu hizo. Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia Mh. Abdulrahaman A.Alli alimteua ndugu RICKY JOHNSON GEORGE BONDO kuwa katibu muwakilishi wa jumuiya ya Watanzania tawi la GENOVA, pia ndugu ZACHARIA MHESA aliteuliwa kuwa katibu mwakilishi wa PADOVA na VENEZIA

No comments:

Post a Comment