J
Mshindi wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010 Diamond alipokea kichapo nje ya ukumbi wa st.dominic Iringa baada ya kutaka kumpiga DJ Muba na msanii wa vichekesho Athuman Mussa a.k.a Mwalubadu .Diamond alifikia hatua hiyo ya kufanya fujo kubwa katika ukumbi huo baada ya kumaliza kuimba na kushuka jukwaani na akiwa nje ya ukumbi huo alimtukana matusi ya nguoni kwa kutumia ishara ya kidole Mbarouk Salum maarufu kama DJ Muba ambaye alikuwa akipinga muziki katika ukumbi huoHatua ya msanii huyo kumtukana DJ Muba ilionyesha kuwakwaza mashabiki wa DJ huyo ambao wamekuwa wakimtegemea katika tasnia ya burudani ndani ya mkoa wa Iringa kwa kupitia kituo cha Radio Ebony Fm na ukumbi wa club V.I.P wa mjini hapo, hali iliyopelekea mashabiki hao kuanza kumshambulia msanii huyo Diamond kwa kumwita mchanga sana katika sanaa hiyo na kuwa tuzo ya Kilimanjaro isimfanye matawi ya juu pamoja na kumweleza ukweli kuwa DJ Muba ni maarufu mara 100 kwake hivyo asitake kujifanyanisha na DJ huyo kauli zilizomkwaza msanii huyo Diamond.
Monday, May 24, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment