KARIBUNI KIWANJA

Monday, May 10, 2010

SLIM AZIKWA LEO ROME


Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy Mh.Abdulrahaman A.Alli akiongea na Watanzania waliohudhuria mazishi ya marehem Salim Issa Isihaka.Mwenyekiti aliwashukuru wote waliohudhuria mazishi na wote ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria,pia aliwashukuru wote waliojitolea kwa hali na mali katika kufanikisha mazishi ,mwenyekiti alisisitiza umoja na ushirikiano zaidi baina ya watanzania.mwenyekiti pia aliushukuru ubalozi wa Tanzania Rome kwa kuhudhuria mazishi na kuwa karibu na jumuiya ya watanzania Italia na watanzania kwa jumla.Mazishi yaliongozwa na Sheikh Rajab Maulidi wa jumuiya ya watanzania tawi la Modena.




No comments:

Post a Comment