KARIBUNI KIWANJA

Tuesday, May 18, 2010

CHIDI BENZ AUKWAA MSAFARA WA KIONGOZI


Mapema leo mchana Msanii bora wa hip hop wa tuzo za Kili Music Awards 2010,Chid Benz amekumbana na sekeseke la polisi maeneo ya Kilwa Road mara baada ya kudiawa kuingilia msafara wa kiongozi mmoja aliyekuwa akipita eneo hilo,hivyo polisi wa usalama barabarani wakamshikilia Chid Benz huku wakimhoji ni kwa nini ameingilia msafara, lakini kwa upande wa mashuhuda pamoja na yeye Chid Benz amedai kutukanwa tusi zito na mmoja wa polisi wa usalama barabarani ndio kukaibuka timbwiri hilo,kufuatia vute nikuvute hiyo Chid Benz akaamua kwenda kutoa taarifa ya kutukanwa kwenye kituo cha Kilwa road

No comments:

Post a Comment